SCCULT (1992) Ltd inawataarifu wanachama wake wote kuhusu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Ishirini na Tisa (29) wa Wanachama wa SCCULT (1992) Ltd, utakaofanyika tarehe 03 Disemba, 2026 katika Cate Hotel, Morogoro, kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi.
About the 29th Annual General Meeting
Mkutano Mkuu wa Mwaka ni jukwaa muhimu la kikatiba linalowakutanisha wanachama wa SCCULT (1992) Ltd kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji, usimamizi na maendeleo ya Chama.
Mkutano huu utatoa fursa kwa wanachama kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Chama, kupitia taarifa za kifedha, kutathmini maamuzi ya mikutano iliyopita na kuweka mikakati ya kuimarisha utendaji na maendeleo ya SCCULT (1992) Ltd.
Key Meeting Agendas
Mkutano Mkuu wa Ishirini na Tisa (29) utajadili na kufanya maamuzi kuhusu masuala muhimu yafuatayo:
- Opening of the Meeting – kufungua Mkutano Mkuu.
- Confirmation of Quorum – kuthibitisha akidi ya Mkutano Mkuu.
- Approval of the Agenda – kuthibitisha ajenda za Mkutano Mkuu.
- Previous Meeting Minutes – kupokea, kujadili na kutolea uamuzi muhtasari wa Mkutano Mkuu wa 28 uliofanyika tarehe 03 Oktoba, 2025.
- Matters Arising – kujadili na kutolea uamuzi masuala yaliyotokana na Mkutano Mkuu wa 28.
- Board Report – kupokea, kujadili na kutolea uamuzi taarifa ya Bodi inayoishia tarehe 30 Septemba, 2026.
- Audit Report – kupokea na kujadili taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Chama zinazoishia tarehe 31 Disemba, 2025.
- Annual Work Plan and Budget 2027 – kujadili na kuidhinisha mpango kazi na bajeti ya mwaka 2027.
- Debt Limit Applications 2027 – kupokea, kujadili na kutolea maamuzi maombi ya ukomo wa madeni kwa mwaka 2027.
- Appointment of External Auditor – kuidhinisha Mkaguzi wa Nje wa Hesabu za mwaka 2026.
- Any Other Business (AOB) – kujadili mambo mengine yatakayowasilishwa.
- Closing of the Meeting – kufunga Mkutano Mkuu wa Ishirini na Tisa (29).
Who Should Attend?
Mkutano huu unawalenga wanachama wa SCCULT (1992) Ltd pamoja na wajumbe watakaowakilisha SACCOS wanachama. Kila SACCOS mwanachama inapaswa kuhakikisha wajumbe wake wanashiriki katika Mkutano Mkuu kwa mujibu wa taratibu na masharti ya Chama.
Meeting Details
- Event: 29th Annual General Meeting of SCCULT (1992) Ltd.
- Date: 03 December 2026.
- Time: 3:00 AM (Saa tatu asubuhi).
- Venue: Cate Hotel, Morogoro, Tanzania.
- Organiser: SCCULT (1992) Ltd.
Important Information for Member SACCOS
Kila SACCOS mwanachama inatakiwa kuwagharamikia wajumbe wake kwa nauli na posho za kujikimu kwa viwango vinavyotumiwa na SACCOS husika.
Gharama za chakula, vinywaji na shajala wakati wa Mkutano zitagharamiwa na SCCULT (1992) Ltd.
Strengthening Member Participation and Institutional Governance
Kupitia Mkutano Mkuu huu, SCCULT (1992) Ltd inalenga kuimarisha ushiriki wa wanachama katika maamuzi ya Chama, kuongeza uwazi na uwajibikaji, pamoja na kuweka mikakati ya maendeleo endelevu kwa mwaka 2027 na miaka inayofuata.
“PAMOJA NA SALAMU ZA SACCOS”
Ushiriki wa kila SACCOS mwanachama ni muhimu katika kujenga Chama imara, chenye uwazi, uwajibikaji na maendeleo endelevu.
Dkt. Lucy M. Kamptoni
Mwenyekiti wa Bodi