ZIARA YA MAFUNZO DODOMA

Chama kikuu cha Ushirika wa akiba na mikopo kiliandaa ziara ya kutembelea vyama kwa nia ya kujifunza na kutimiza Misingi ya Ushirika wa tano na sita (Elimu, Mafunzo , taarifa pamoja na kushirikiana baina ya vyama vya Ushirika)

Ziara hiyo imefanyika mkoa wa Dodoma tarehe 13 hadi 15 Disemba 2022 na kuhudhuriwa na vyama mbalimbali kutoka mkoa wa Dar es salaam, Mbeya, Kilimanjaro pamoja na Tanga.

Lengo la ziara hii ni kubadilishana uzoefu, kujifunza na kufahamu taasisi zinazotusimamia. Washiriki walifanikiwa kutembelea Ofisi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Shirika la ukaguzi katika vyama vya Ushirika (COASCO), Chuo kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Dodoma (MoCU) Tanzania Mentors Action (TMA), KKKT Arusha Road SACCOS, URA SACCOS Dodoma Branch, TCDC SACCOS LTD, Ukaguzi A.S.F SACCOS pamoja na TMA SACCOS.

Mafunzo haya yamejenga wigo wa uelewa kwa washiriki na waliotembelewa na hivyo kupata nafasi ya kuboresha SACCOS.

administrator