- Napenda kuwataarifu kuwa kutakuwa na Uchaguzi wa Viongozi wa Bodi ya SCCULT (1992) Ltd katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Ishirini na saba wa wanachama wa SCCULT (1992) Ltd utakaofanyika tarehe 25 Oktoba, 2024 jijini Mwanza katika ukumbi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (MWAUWASA) jijini Mwanza.
- Kwa wale ambao watavutiwa kuomba nafasi za Uongozi wanatakiwa kuhakikisha majina yao yametambuliwa na SACCOS zao kama wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SCCULT (1992) Ltd na kujaza vizuri fomu na kuwasilisha pamoja na viambatanisho vingine (Wasifu na nakala zilizo dhibitishwa za vyeti vya elimu na vingine vitakavyohitajika). Fomu pamoja na viambatanisho viwasilishwe kwenye Ofisi za SCCULT (1992) Ltd Makao Makuu (Jengo la Ushirika, Ghorofa namba 16) au kwenye Ofisi za Warajis Wasaidizi au Maafisa Ushirika.
- Vyama wanachama wa SCCULT (1992) Ltd mnapaswa kuzingatia taratibu zote za Uchaguzi kama zilivyoelekezwa na Sheria, Kanuni na Masharti. Aidha kutekeleza taratibu za ulipaji wa ada ya mwaka, uwekezaji na michango mingine yote iliyoamuliwa na Mikutano Mikuu ya wanachama.
- Wote Mnakaribishwa kwa taarifa zaidi bonyeza hapa kupata tangazo hilo na pia unaweza bonyeza hapa kupata fomu ya maombi.