Chama kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SCCULT) (1992) Ltd., kwa kushirikiana na wadau wake, Shirika la DSIK-Tanzania, kimeendesha mafunzo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa wanachama wa Chama cha SHIWARA SACCOS Ltd. Mafunzo haya yanafanyika kuanzia Mei 21 hadi 24, 2024, wilayani Arumeru, Jijini Arusha.
Mafunzo haya ni sehemu ya juhudi za SCCULT (1992) Ltd. na DSIK-Tanzania katika kuwajengea uwezo wanachama wao, hususan wakulima, kuhusu jinsi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zinaweza kuathiri shughuli za kilimo. Mada zilizojadiliwa ni pamoja na umuhimu wa bima katika kilimo na mbinu za kubuni bidhaa mpya ambazo zitavutia watu nje ya sekta ya ushirika kujiunga na kunufaika na sekta hii.
Washiriki wa mafunzo haya wameishukuru SCCULT (1992) Ltd. na DSIK-Tanzania kwa jitihada zao katika kuwajengea uwezo na kuboresha shughuli za vyama vya ushirika na wanachama wake.
#SCCULT jumuishi kwa ustawi wa SACCOS